Watu ishirini walipanda juu ya mti, wawili wakaona chungwa, watano wakalichuma, kumi wakalimenya, wote wakaridhirika mtu mmoja alile. Je, ni watu gani hao? jibu Waliopanda ni vidole vya miguu na mikono, walioona ni macho mawili, waliochuma ni vidole vitano vya mikono, waliomenya ni vidole vya mikono yote miwili, na aliyelila ni mdomo