Msingi wa Fasihi Simulizi By Kingei

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Msingi wa Fasihi Simulizi By Kingei Details


Msingi wa Fasihi Simulizi ni Kitabu kinachozitalii kwa upana dhana za kimsingi katika utanzu wa fasihi simulizi. Kitabu hiki kinawapa wanafunzi na walimu wa fasihi simulizi kwa Kiswahili msingi jadidi katika taaluma hii. Vipera mbalimbali vya fasihi simulizi vimefafanuliwa kwa undani huku mifano maridhawa ikitolewa kutoka jamii anuwai barani Afrika na kwingineko. Istilahi kadhaa zinazotumiwa katika uchambuzi wa fashihi simulizi zimejadiliwa kwa namna ya kipekee. Maswali ya kudurusu yametolewa ili kumhami vilivyo mwanafunzi wa fasihi simulizi. Kitabu hiki kitawafaidi wanafunzi, walimu, wasomi na wapenzi wa fasihi simulizi kuanzia shule za upili hadi vyuo vikuu. Waandishi; Prof. Kitula King'ei na Bi. Catherine Kisovi ni walimu na wataalamu wenye tajriba pana katika uandishi na ufundishaji wa Kiswahili katika viwango mbalimbali. ISBN: 9966446001 SKU: 2010143000111