Haini By Adam Shafi

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Haini By Adam Shafi Details


Hamza, kijana mwandishi wa habari, anakamatwa kwa kutuhumiwa kuwa haini, hasa kutokana na uhusiano wake wa karibu na Hamduni, ambaye amempiga risasi na kumwua Kigogo, kiongozi wa nchi. Sehemu kubwa ya riwaya hii inasimuliwa gerezani ambako Hamza pamoja na wengine waliosombwa na kurundikwa huko, wanateswa, kuthakilishwa na kutendewa unyama wa kila namna.Haini ni riwaya inayochukua tukio la kihistoria la kuuawa kwa kiongozi mmoja wa Kiafrika mwaka 1972, na kulifanya kiini cha kuyachunguza matatizo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi za Kiafrika baada ya uhuru, chini ya mifumo ya utawala inayojali tu maslahi ya wachache. Ni riwaya yenye uhisivu na taharuki ya kipekee, na licha ya kuwa na sifa za kitanzia, inasheheni msambao wa ucheshi na viliwazo."Alinyanyuliwa akatupwa nje na baada ya kutua juu ya ile sakafu tu wakam'mwagia ndoo nzima ya maji kumfufua arudi tena duniani. Walipomwona anazindukana wakaanza tena, 'sasa utasema'."

ISBN: 9789966497666 SKU: 2010143000054