Hadithi za Furaha Kitabu Cha 1 By Kingei

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Hadithi za Furaha Kitabu Cha 1 By Kingei Details


Hiki ni kitabu cha kwanza katika mfululizo wa vitabu vya hadithi unaoitwa Hadithi za Furaha. Vitabu hivi vimedhamiriwa kutumiwa na wanafunzi wa madarasa ya nne hadi ya nane katika shule za msingi. Kusoma ni njia moja muhimu katika kujifunza lugha yoyote. Hadithi zilizomo zimechaguliwa na kutayarishwa iii kutimiza mahitaji ya wanafunzi wa viwango hivi. Mahitaji haya ni pamoja na kuinua kiwango cha ujuzi wa lugha na uwezo wa kusoma na kufahamu. lsitoshe, vitabu hivi vimekusudiwa kuimarisha maadili ya wasomaji wake kama bidii, uaminifu, mapenzi, utiifu na kadhalika. Hadithi zote zimeandikwa kwa njia ya kuwavutia na kuwapendeza wasomaji pamoja na kuwapa mafunzo yafaayo. Kitula G.King'ei ambaye ni mwalimu wa kiswahili amewahi kuchapisha vitabu kadhaa vya somo la kiswahili. Baadhi yake ni Mwongozo wa Malimwengu Ulimwenguni, Mwon-gozo wa Malenga wa Mrima na Mwongozo wa Mashetani. 

ISBN: 9966441743 SKU: 2010143000250