masomo ya msingi 7 ni kitabu cha saba katika mfululizo wa vitabu vinane vya Kiswahili katika Shule za Msingi. Kila kimoja cha vitabu hivi kinakuza masomo ya kitabu kinachofuata. Vitabu hivi vimeandikwa upya kulingana na matarajio ya ratiba iliyotolewa na Taasisi ya Elimu (2002). Michoro iliyomo katika kitabu hiki ni ya kupendeza kwa kila mwanafunzi anayejifunza Kiswahili. Kitabu hiki kinafundisha lugha kutegemea stadi na maarifa kama inavyopendekezwa na Taasisi ya Elimu ya Kenya. Mifano iliyotolewa ni ile ambayo mwanafunzi anakumbana nayo katika maisha yake ya kila siku. Masomo katika Masomo ya Msingi 7 yamepangwa kulingana na mgawo wa stadi zilizoko kwenye silabasi. Kila sura katika kitabu hiki imegawika kama ifuatavyo: A. Ufahamu B. Msamiati C. Sarufi D. Kusikiliza na kuongea E. Kuandika Kitabu hiki kimejengwa katika misingi thabiti ya hatua kwa hatua, hali ambayo itamwezesha mwanafunzi kusoma taratibu na katika hail ya kujiendeleza. Mna pia mazoezi ya kutosha ya kumjenga mwanafunzi ipasavyo. Waandishi wa mfululizo huu wa Masomo ya Msingi ni wenye tajriba kuu katika ualimu na wanayafahamu mahitaji ya wanafunzi waliowaandikia. Ni matumaini yetu kwamba mfululizo wa masomo haya utakuwa mwangaza kwa wote.
ISBN: 9966341714 SKU: 2010124000161