Mkondo wa maisha By Ali H.Njama

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Mkondo wa maisha By Ali H.Njama Details


Hakika mkondo wa maisha ni kitu kigumu sana. Kwani maisha yamegawanyika mikondo ya tabaka mbalimbali, sawa na ile mikondo ya bahari. Unaweza kuupata mkondo wakati vva shuari ukatamani ushinde, au ukeshe humo baharini. Lakini pindi ukikuchafukia na kukumbana na kimbunga na pepo za maghibu, unaweza kula kiapo kama hutakanyaga bahari maisha. Lakini kwa ushujaa na ukakamavu wa binadamu, hukabiliana na tufani hizo, kila uchao yu mumo akitafuta riziki yake. Ilinibidi nikabiliane nayo mashaka kama vile wayakabiliavyo watu wema. Mkondo wa Maisha ni riwaya inayowaasa vijana kutojiingiza kwenye mapenzi ya chati. Pia inafunza waru saburi wanapokumbana na mashaka ya dunia. Mtiririko wa hadithi hii ni wa usimulizi.

ISBN: 9966221719 SKU: 2010143000091