Sahani ya Hoho By One planet

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Sahani ya Hoho By One planet Details


Alikuwa amelia machozi yote. Alikuwa ameomba dua zote. Alikuwa amepigwa mara elfu. Alikuwa amefanyiwa kila lililo baya. Mabaya na maovu ambayo yalikuwa yamevunda na kunuka fee hata shetani mwenyewe angepewa. angechana mbuga. Angetoroka na kuyakana. Angekimbia bila roho yake ...Ni kweli maisha hayana ladha kamili ya maisha; uchachu umekulula. Kama huamini,nenda ukamwulize Shukran. Safari yake katika maisha ina changamoto si haba. Kila hatua anayoipiga anapata ameandaliwa mlo mtamu, utamu mchungu na mkali. sahani ya hoho, Sahani hii hakuna wa kumwondolea ila yeye mwenyewe. Je siri yake ni gani?

ISBN: 2010143000789 SKU: 2010143000789