Kiswahili Kwa Darasa la 6 By

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Kiswahili Kwa Darasa la 6 By Details


Hili ni toleo la pili la Kiswahili kwa Darasa la Sita. Kitabu hiki cha wanafunzi ni cha sita katika mfululizo wa vitabu vinane vya lugha ya Kiswahili kwa shule za msingi. Kitabu hiki kimefanyiwa marudio kwa mujibu wa silabasi mpya ya Kiswahili ya 2002 ya Darasa la Sita. Katika toleo hili, maswala nyeti yameshughulikiwa kama vile, mpangilio mpya wa ngeli na maswala ibuka kama vile ukimwi, ajira za watoto, mazingira na maadili. Mifano, michoro na picha nyingi zimetumiwa ili kufanya somo hili liwe la kuvutia zaidi. Mazoezi kemkem yamejumuishwa ili kumhusisha mwanafunzi kikamilifu. Ni kitabu ambacho wanafunzi watafurahia kukitumia. Vitabu vifuatavyo vya Kiswahili, ambavyo vimechapishwa na KLB pia vyapatikana katika mfululizo huu: