Hili ni toleo jipya la Kiswahili kwa Kidato cha Nne, Kitabu cha Wanafunzi. Kitabu hiki ni cha nne katika mfululizo wa vitabu vinne vya Kiswahili kwa shule za upili. Kitabu hiki kimefuata mfumo wa elimu wa 8-4-4 na kufanyiwa marudio kulingana na silabasi mpya ya Kiswahili ya 2002 ya Kidato cha Nne. Katika toleo hili, maelezo zaidi juu ya nyanja mbalimbali za lugha yameshughulikiwa kama vile, mpangilio mpya wa ngeli, kusoma kwa kina, na msamiati na istilahi kimuktadha. Pia, maswala ibuka kama vile maadili, UKIMWI na mazingira yamejitokeza. Mifano zaidi, michoro na picha zimetumiwa ili kufanya somo hili liwe la kuvutia. Ni kitabu ambacho wanafunzi watafurahia kukitumia.