Nadharia za Uhakiki wa Fasihi ni kitabu kinachoshughulikia nadharia za uhakiki na utendakazi wake. Katika kitabu hiki waandishi wanaainisha nadharia za uhakiki wa fasihi, kuonyesha mihimili yake, na jinsi nadharia hizo zinavyotumika kufafanua kazi za sanaa. Kitabu hiki kitawafaa walimu wa shule za upili, wanafunzi na wahadhiri wa vyuo vikuu, na wapenzi wote wa fasihi ya Kiswahili.