Tunu ya Ushairi ni mkusanyo wa mashairi ya aina, maudhui na mitindo mbalimbali. Kuna mashairi arudhi, mashairi huru na mashairi picha. Diwani hii ina mashairi ambayo msomaji atajihusisha nayo kwa njia rahisi. Ujumbe wake unapitishwa kwa njia sahili na yenye mguso unaoiacha athari ya kudumu kwa msomaji. Washairi hawakujikita katika mikondo iliyopo tu; wamezuka na mikondo mipya ya utungaji wa mashairi arudhi ambayo itachangia kubadilisha mtazamo wetu kuhusu aina za mashairi. Mkusanyo huu unatoa changamoto kwa wahakiki wa fasihi kutathmini upya maelezo yao kuhusu dhana mbalimbali za ushairi.