Maisha Kitendawili By

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Maisha Kitendawili By Details


"Mahaba ni mithili ya kondo; yakushikapo yanakutia donda. Penzi la Farida kwa Kim limegeuka na kuwa pendo. Farida sasa katota..." Itakuwaje? Riwaya hii ya kusisimua inatuingiza katika bahari tesi ambamo asiyesimama imara huzama ji! Unapoisoma unachukuliwa na wimbi la vitushi vya hadithi iliyotambwa kwa ufundi wa kipekee. Maisha Kitendawili ni riwaya ya pili ya Dkt. John Habwe. Riwaya yake ya kwanza, Maumbile si Huja, imewafurahisha wapenzi wa fasihi ya Kiswahili, si haba. Pia, ameandika hadithi fupi kama vile "Pendo la Heba " na "Walicheka Kicheko". Mwandishi amejibainisha kuwa na uketo wa lugha ya Kiswahili na uelewa mpana wa matukio na mitagusano inayopitikia jamii za kisasa. Mwalimu Habwe ni mtaalamu wa Isimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi.