Bina-Adamu ni riwaya inayotumia sitiari ya kijiji kuangalia hali ya mataifa ya ulimwengu katika kipindi hiki ambapo hali za kijamii, kisiasa na kiuchumi zinadhibitiwa na ubepari wa mataifa yaliyoendeiea. Hii ni riwaya changamano yenye ufundi wa lugha na wa kimtindo. lnamfanya msomaji awazie sio tu yanayozungumziwa ball pia muundo wa riwaya ya kiswahili.