Mchimba Madini By

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Mchimba Madini By Details


Mchimba Madini ni hadithi ya awali aliyoiandika Peter Abrahams. Hadithi yenyewe ni juu ya Xuma; kijana wa mashambani aliyekuja kuishi katika jiji kubwa Ienye viwanda vingi nchini Afrika Kusini. Maisha haya yanamfunulia mbinu mpya za kuishi. Ukweli ni kwamba mwandishi anamwelezea Xuma kama mtu aliye katika mabadiliko. Anamtumia Xuma kama chombo chake cha kuyaelezea maisha ya watu wa chini jijini. Kwa sababu Xuma ni mgeni katika maisha haya, ugumu na masumbuko ya maisha haya ya chini kwake ni kitu kipya kabisa. Hiki kilikuwa kitabu cha kwanza kabisa kilichofichua ugumu wa maisha ya Waafrika wa Afrika Kusini chini ya utawala wa weupe wachache.