Dunia Yao ni riwaya inayothibitisha namna ujasiri wa mwandishi ulivyoimarika kwa kujadili mambo nyeti kuhusu jamii yake na mataifa. Tunakutana na Ndi- anayejifungia njozini kukimbia ukweli unaompa mateso na kuihangaisha akili yake. Mwishowe anaishiwa na kila kitu ila ishara za mauti. Kwa nini? Kitendawili hiki tunakuachia wewe msomaji ukitegue. Ulimwengu wa riwaya hii na msuko wake, na umbo lake na muundo wake, kamwe si wa kawaida. Umetengenezwa kumvutia msorraji kwa njia ya ajabu. Ni wa majaribio yanayovunja sarufi au kanuni zote za lugha na sanaa iii ufanane na dunia tunayoishi leo. Dunia ambayo ni tata na ovyo, iliyobutuka, iliyoparaganyika, inayotuchezesha foliti za mauti, inayonata utamu wa kifo na uchungu wa uhai. Inamtafuta msomaji imnase mara anapokikamata kitabu.