Kiswahili Angaza, Mwongozo wa Mwalimu, Gredi ya 5 ni kitabu kilichosukwa na kuwambwa kwa makini na kwa kina kirefu. Kimetimiza kwa ukomo wa ukamilifu mahitaji ya Mtalaa wa Kiumilisi. Mwongozo huu unafafanua yaliyomo katika Kiswahili Angaza, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 5. Mwongozo huu unatoa mwelekeo ufaao kwa mwalimu na kumwongoza hatua kwa hatua katika ufundishaji. Mwongozo huu unajumuisha:
• Utangulizi unaofafanua kwa kina vipengele muhimu vya mtalaa wa umilisi.
• Kielelezo cha maazimio ya kazi pamoja na andalio la somo kwa kutumia mtindo uliopendekezwa na KICD.
• Mapendekezo ya jinsi ya kushughulikia wanafunzi wenye mahitaji ya kipekeedarasani.
• Utangulizi kwa kila mada. Kabla ya vipindi vyenyewe, mwalimu anaonyeshwa matokeo tarajiwa maalum ya kila mada; umilisi wa kimsingi unaokuzwa; uhusiano wa mada na masuala mtambuko, maadili na masomo mengine; mapendekezo ya shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji; nyenzo za kufundishia na mbinu za kutathmini wanafunzi.
• Mwongozo wa kutekeleza kila shughuli iliyo kwenye kitabu cha Mwanafunzi hatua kwa hatua.
• Majibu kamili ya mazoezi pamoja na maelekezo kwa mwalimu kuhusiana na shughuli teule
• Viwango vya mwalimu kuzingatia anapowatathmini wanafunzi wake. Mwongozo huu umeandikwa kwa utaalamu na waandishi wenye uzoefu mwingi.