Mwinyi anapozaliwa anakuwa tumaini la mamake; la kumpoza moyo katika ndoa ya lazima. Anaasi ushauri hata hivyo na kuishia kuwa mhuni. Hatimaye anachupia meli ya kwenda Uarabuni ili kutafuta uhuru wa kufanya anavyotaka na kuishi maisha ya raha mustarehe, yasiyo na kero wala tafrani. Je, atafanikiwa kuyapata maisha haya? Hadaa ya Nafsi ni hadithi yenye kusisimua na inayogusa msomaji hasa anapoyatafakari maisha ya Mwinyi, mamake, babake na rafiki yake, Shaka.
ISBN: 9789966229953 SKU: 2010143000787