Onyo la Mwisho By Zake Yaona

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Onyo la Mwisho By Zake Yaona Details


Tazama ushahidi nilio nao hapa. Eti ni kifo cha KD: kinyago, askari na watoto washukiwa. Washukiwa ambao hata sijui wanashukiwa kuiba au kufanya nini... "Wallahi KD atajua kuwa sikuenda Kiganjo kuuza njugu karanga wala kuuza mayai!" Inspekta Kausi aliapa. KD amezivuruga akili za Inspekta Kausi kupita maelezo. Jambazi hilt hatari limeamua kuucheza mchezo ambao inspekta ameuvalia njuga. Je, kikosi cha inspekta kitamtia KD mbaroni? KD ambaye kumkamata ni kama kuitafuta rangi ya upepo? Riwaya hit itakufichulia kisasi kibivu, mapenzi hatari, tamaa mbichi, maonyo mekundu, upelelezi motomoto, hasira baridi, na uongo wa ukweli na ukweli wa uongo. 

 

ISBN: 9789966068422 SKU: 2010143000872