Utamu wa Kiswahili: Shughuli Mzomzo, Gredi ya 3 ni hatua adhimu katika safari ndefu ya kuitalii lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki ni hatua muhimu ya kwanza katika kutambua kipawa cha mwanafunzi na kupalilia ilhamu ya fanaka katika maisha yake.
Mambo yaliyomo yamepangwa kwa lugha nyepesi iliyojaa ubunifu na burudani. Mifano iliyotolewa ni ya kumwezesha mwanafunzi kuhisi uhalisi na uhai wa mazingira yake. Mpango uliotumika unamfanya mwanafunzi kujihisi kuwa sehemu ya kazi Yenyewe na kwa hivyo kuimarisha umilisi wa shughuli na kutimiza malengo ya kiwango, malengo maalum na malengo ya kijumla.
Utamu uliokolea hasa katika:
1. Shughuli za binafsi.
2. Shughuli za vikundi.
3. Shughuli za makundi.
4. Shughuli za utafiti na utaftishi.
5. Shughuli za kijamaa.
6. Shughuli za kijamii. Sa
7. Shughuli kumbukizi.
Utamu wa Kiswahili ni kitabu kinachofanya kumjenga mzalendo anayetarajiwa kuitetea na kuijenga nchi kwa dhati ya moyo.
Ni suluhu kwa ujifunzaji wa Kiswahili.
Usichelewe kugonga gogo kupata utamu wa mlio!
ISBN: 9789966101440 SKU: 2010127000764