OUP Kiswahili Dadisi GD3 Trs (Approved) By Nyaga

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

OUP Kiswahili Dadisi GD3 Trs (Approved) By Nyaga Details


Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa njia ya kipekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa umilisi. Vitabu katika msururu huu vitamwezesha mwanafunzi kupata umilisi wa lugha katika stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika kama ilivyopendekezwa katika mtalaa mpya.

Vitabu katika msururu vina mazoezi murua ambayo yatamchangamsha muwanafunzi na kumpa hamu ya kutaka kujifunza lugha. Mazoezi haya yanakuza umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masualaibuka. Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Mwongozo wa Muwalimu, Gredi ya 3 kina mifano halisi na ya kutosha kumwezesha mwalimu kuwasaidia wanafunzi kukuza umilisi unaokusudiwa. Katika mwongozo huu utapata:

 

  • utangulizi wa kina kuhusu mtalaa huu mpya wa umilisi
  • muhtasari wa umilisi, maadili, masualaibuka na shughuli nyinginezo zilizoratibiwa kufundishwa katika kila sura
  • matokeo maalumu, maandalizi ya somo na shughuli za ufunzaji wa kila somo
  • mapendekezo ya majibu ya maswali yote katika Kitabu cha Mwanafunzi
  • mapendekezo ya shughuli za wanafunzi nje ya darasa
  • maelekezo ya king kuhusu jinsi ya kutathmini wanafunzi.

 

Kiswahili Dadisi, Mazoezi ya Lugha, Kitabu cha Mwanafunzi pamoja na Mwongozo wa Mualimu ving shughuli, mazoezi na maelekezo tosha ambayo mwanafunzi na mwalimu watahitaji ili kufaulu katika mtalaa huu mpya wa Umilisi.

ISBN: 9780195746877 SKU: 2010127000726