Zipo hadithi za kale, za mnyama aliyeitwa 'Nunda’ ambaye anaelezewa kuwa alikuwa mla watu. Watu walizichukulia hadithi hizo kama za mapokeo, zisizo na ukweli wowote. Lakini pale 'Nunda Mla Watu alipoibuka jijini Dar es Salaam na kuanza kuteketeza maisha ya watu mbalimbali, kila mtu aliingiwa na hofu.
Upelelezi mkali wa polisi unagonga mwamba na hivyo kufanya vifo viendelee kutokea. Aidha barua za vitisho zenye sahihi ya Nunda zinaendelea kuwaendea watu. Zikiwataka kufuata masharti yake. Wanaokataa kumtii wanapoteza maisha.
Joram Kiango anaingilia kati. Lakini upelelezi wake unamfanya kila hatua anayopiga impeleke karibu zaidi na domo la Nunda huyo, lililo wazi, likimsubiri kwa hamu.
ISBN: 9789966256294 SKU: 2010143000644