Kiswahili Dadisi ni msururu wa vitabu vipya vilivyoandikwa kwa upekee ili kutosheleza mahitaji ya mtalaa mpya wa umilisi. Vitabu hivi vitamwezesha mwanafunzi kupata ufahamu wa lugha kupitia stadi za kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika, na vilevile sarufi. Aidha, vina mazoezi murua ambayo yatampa mwanafunzi hamu ya kujifunza.
Pia vinakuzo umilisi uliopendekezwa, maadili na kufahamisha kuhusu masuala ibuka.