Hadithi hii inayazungumzia maisha halisi ya mwandishi katika utoto na ukuaji wake.
Akiwa mdogo yeye ndugu zake ni wajeuri, wasiopenda kuoga na wasumbufu walivyo watoto wengine wa umri mdogo katika jamii.
Umaskini unawasakama mwandishi na familia yake. Shore ambaye ni mwanambee katika familia ya mwandishi,
anafanikiwa kupata ajira nzuri mjini Mbuta kutokana na kisomo chake.
Anaifaa familia yake kwa kila namna hadi pale maisha ya kila mmoja katika familia hii yanakuwa rahisi na mazuri.
Safiri nami katika kuisoma hadithi hii ya kukata na shoka.