Basi babu akaingia kwenye gajabu na kutoa bunduki moja.
Kisha kwa ghafla akaona selidamu nyekundu moja iliyoingiwa na vimelea wa malaria.
Babu akaruka akawafyatulia kemikali vimelea wa malaria. Vimelea wakapiga mayowe na kuanguka nje ya selidamu
wakiwa wamekufa tayari! Je, safari ya babu na Makumba ndani ya mwili wa mwanadamu itafua dafu?
Msururu wa Makumba ni novela bunilizi za kisayansi za kusisimua ambazo zinatalii sayari,
mwili wa binadamu, ndani ya mimea na hata ndani ya ncha ya kalamu.
Dkt. Hamisi Babusa ni mhadhiri wa Kiswahili na Taaluma ya Ufundishaji Lugha katika Chuo Kikuu cha Kenyatta.
Ni mwandishi ambaye amechangia katika nyuga mbalimbali za uandishi bunilizi na za kiakademia.
Miongoni mwa kazi zake nyingine ni Makumba katika Safari ya Mawimbi, Makumba katika safari ya Tonge,
Makumba na Majanabi na Makumba katika Siri ya Mwembe.