Gajabu ikanguruma vizuri. Kisha kwa upesi sana, Makumba akachapa neno
'sikioni kwenye kidubwasha cha kukotoa kisha akabofya kitufe cha kukubali.
Gajabu ikainuka juu na ikaanza kuzunguka kwa kasi sana huku iklanza kuwa ndogo.
Makumba alizimia ndani ya gajabu. Ungana na Makumba kwenye
safari ya utalii wa ndani ya sikio la mwanadamu. Msururu wa Makumba ni novela
bunilizi za kisayansi za kusisimua ambazo zinatolil sayari mwili wa binadamu,
ndani ya mimea na hata ndani ya ncha ya kalamu Dkt Hamis Babuso ni mhadhiri wa Kiswahili na
Taaluma ya ufundisha Lugha katika Chuo Kikuu cha Kenyatta Ni mwandishi ambaye
amechangia katika nyuga mbalimbali za uandishi bunilizi na za
lahadema. Miongoni mwa kazi zake nyingine ni Malumba na Selidamu Nyeupe,
Makumba katika Safari ya Tonge. Makumba na Majanabi na Makumba katika Siri ya Mwembe