Kusoma na kuandika katika Kiswahili, Gredi 1 ni kimoja miongoni mwa vitabu vipya
vilivyoandikwa kwa kuzingatia mtaala mpya unaokuza ujuzi wa wanafunzi kupitia kwa utendaji na uvumbuzi wa maarifa.
Kitabu hiki kinawawezesha wanafunzi kupata maarifa ya kimsingi,
stadi zifaazo za kusoma na kuandika, mienendo miema na maadili ya kimaisha
pamoja na utumizi kamili wa maarifa wanayoyapata darasani.
Shughuli na mazoezi katika kitabu hiki zimejikita kwenye uzoefu wa wanafunzi wa kila siku
pamoja na masuala ya kisasa na ibuka kama yalivyofafanuliwa kwenye mtaala mpya.
Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha rahisi na inayoibua tafakari tanduizi ili
kukuza ujuzi wa kutafakari na kuimarisha stadi za kimaisha za usuluhishaji wa matatizo ili kukidhi
mahitaji ya wanafunzi katika jamii.