Jahazi la Insha shule za Msingi By Mwalimu Simba

by sava in Text book centre buy now Publishered by: sava

Jahazi la Insha shule za Msingi By Mwalimu Simba Details


TOLEO hili la JAHAZI LA INSHA ni kitabu kilichoandikwa kwa uangalifu, 
umahiri na ustadi wa hali ya juu. Tofauti na vitabu vingine vya Insha - kitabu 
hiki kimezingatia mambo yafuatayo kupitia mfumo wa teknoloji-mwandishi wa kitabu hiki 
ametayarisha kanda ya video inayobeba ujumbe wote uliochapishwa kwenye kitabu hiki. 
Mwanafunzi anaweza kutalii mbinu zote za uandishi kupitia njia mbalimbali km kutazama 
kusikiliza kusoma kwa kuipatia (a) nakala ya kitabu cha Jahazi la Insha 
(b) nakala ya video ya jahazi la Insha Jahazi la Inshani kitabu kinachomwezesha
mwalimu kwa mwanafunzi kujenga msingi wa stad ya kuandika kupitia mapambo zaidi ya mia nane 
yanayolenga kukipeva kukiendeleza na kukidumisha kipawa hiki cha uandishi kumbukeni kuwa 
hakuna mwanafunzi anayezaliwa na usani wa uandishi aidha kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba 
yake Mwandishi amejaribu kubuni njia zilizoahisi na sahili kumwezesha mwanafunzi 
kuzielewa aina zote za inshak.m. kupitia jukwaa la mazoezi - kujaza mapengo ya mitungo kadhaa.
Kazi yote iliyotayarishwa katika kitabu hiki imefuata masharti ya silabasi ya shule za msingi kikamilifu.
Kitawaondolea gharama ya kununua vitabu vingi kwa ajili ya uandishi na pili kuwapunguzia walimu 
tatizo la kubukua vitabu vingi ili kutosheleza mahitaji ya uandishi bora wa mitungo ya Kiswahili
 

SKU: 2010127000685