Vitabu vya Sayari vimenuiwa kuwaongezea wanafunzi maarifa ya kusoma na kuielewa lugha ya Kiswahili huku vikiwafanya
wajimudu katika kuizungumza lugha hii.
Vimekusudiwa kusomwa na wanafunzi wa Darasa la Sita, Saba na la Nane katika shule za msingi za Afrika Mashariki.
Kwa kuwa hawa ni wanafunzi waliokomaa, lugha katika mfululizo wa vitabu hivi imepevushwa ili kuwatayarisha kwa mitihani.
Wanafunzi wengi hutamani kutembelea mbuga za wanyama wa pori ili kujionea wanyama wa aina mbalimbali. Hivi ndivyo
alivyokuwa Mkola. Alipoipata nafasi hii baada ya kujaribu juu chini, alifurahi kweli kweli.