Kiswahili Dadisi Workbook ni mfululizo wa kipekee wa vitabu vya mazoezi katika Mtalaa mpya wa Umilisi.
Kila kitabu katika mfululizo huu kimefanyiwa utafiti wa kina na kuandikwa kwa ustadi ili kuwasaidia wanafunzi kupata
umilisi wa kimsingi, ujuzi, maadili na kuwa na mitazamo bora maishani. Vitabu hivi vinatoa utaratibu mwafaka wa kufanya
mazoezi ya lugha kwa njia nyepesi na ya kueleweka. Kitabu hiki:
• kimeandikwa kwa kufuata utaratibu uliopendekezwa kwenye mtalaa
• kina mazoezi mengi ya kuchangamsha na kuelimisha, na ambayo yatamwezesha mwanafunzi kujenga na kupanua umilisi katika kila mada.
• kina tathmini ya binafsi ambayo itamsaidia mwanafunzi kukadiria umilisi wake katika
mada ndogo zote.
Majibu ya mazoezi katika vitabu vyote vya Gredi ya Nne yanapatikana katika kitabu kimoja.